Kwa miaka mingi sasa kumekuwa na farasi katika shamba la Bockgården. Hivi sasa, pamoja na majirani zetu wa Tyskgården tunakuletea kumbukumbu njema za Bockgården. Farasi wanapenda kufanya kazi na ni vizuri sana kuwa pamoja nao!
Kuna mambo mengi mtu anaweza kufanya akiwa na farasi mwema wa ‘nordsvensk´ na aliyefunzwa vizuri. Kwa kutumia farasi na gari yake tutakupeleka Springkällan, kwenye chemchemu ya asili na uzuri uliotanda kwenye hifadhi ya maliasili. Tutakapofika, tutawasha moto na kunywa kinywaji cha moto pamoja na kitafunwa. Tutahisi na kufurahia kwa pamoja majira ya kuchipua.
Wakati wa ziara, unanafasi ya kujifunza zaidi kuhusu farasi na mandhari yetu, ukiwa pamoja na majirani wetu wema na wachangamfu wenye kupenda farasi wa kitamaduni wa ‘nordsvensk’.
Baada ya kurudi ziarani iliyogubikwa na hisia za aina yake, utafurahia chakula kitamu cha Bockgården.
* Chakula ni cha mbogamboga za majani ambapo bidhaa nyingi zao ni za kiekolojia na zimezalishwa ndani ya nchi.
Furushi hili linatolewa siku za wikiendi yaani mwishoni mwa wiki kuanzia mwanzoni mwa Aprili mpaka katikati ya msimu wa kiangazi. Muda wa kujiandikisha ni kuanzia siku ya Ijumaa saa 9 mchana na muda wa kutoka ni siku ya Jumapili sio zaidi ya saa 5 asubuhi.
Bei la furushi hili la likizo ni Krona 3 200 kwa mtu mzima na Krona 2 500 kwa mtoto kati ya umri wa miaka mitatu na miaka kumi na mbili. Watoto chini ya umri wa miaka mitatu ni bure!
Bockgården ni shamba dogo kwa hivyo tunatoa huduma za kipekee na kwa watu wachache. Furushi hili linatolewa kwako tu na wenzako utakaokuja nao. Tunauwezo wa kuchukua watu sio zaidi ya watano kwa pamoja. Chini ya hapo ni watu wawili.
Tunakuhimiza kutumia usafiri wa umma kwa ajili ya mazingira. Tuna hiari kuja kukupokea na farasi na gari yake kutoka kwenye kituo cha reli bila ya gharama za ziada, tujuulishe tu kabla hujaja.
Unaweza kuendelea kukaa Bockgården baada ya furushi hili.
|
Copyright 2012 Naturbruket Siljan |