tanzania_liten.gif spanien_liten.gifengland_liten.gifsverige_liten.gif
Tuelewe Utalii wa Mazingira Furushi la likizo Jinsi ya kufika Wasiliana nasi
logotyp.gif

Bockgaarden.jpg

Bockgården

Bockgården (Bokgoden) ni jina la shamba letu liliopo katika kijiji kimojawapo cha kihistoria kiitwacho Sjurberg (Khurberi). Kijiji cha Sjurberg kipo Kaskazini-Magharibi mwa Rättvik, Uswidi ya kati, Mkoa wa Dalarna. Mbali na vitu vyengine, kijiji hiki ni maarufu kwa dohani zake zilizobuniwa vizuri na utamaduni wake.

Usanifu wa majengo ni mchanganyiko kulingana na vipindi mbalimbali vya maendeleo ambayo kijiji hiki kimepitia. Mwishoni mwa karne ya 19, kuendana na kupanuka kwa reli hadi Rättvik, kijiji kilibadilika ghafla baada ya matajiri wa mjini kuhamia kwa wingi katika mazingira tulivu ya ukanda wa Ziwa Siljan. Kuna vitabu kadhaa vinavyoelezea Sjurberg na mashamba yake likiwemo Bockgården. Kitabu ’Byar och Fäbodar i Rättvik Kommun’ (Vijiji na mashamba ya kiangazi katika Wilaya ya Rättvik) kinaelezea vyema mazingira ya kijiji cha Sjurberg. Kwenye kitabu hicho imeelezwa kwamba shamba lililohifadhiwa vizuri ni Bockgården pamoja na nyumba zake na muundo mzima wa kitamaduni wa majengo ya nje.

Bockgården ipo ukingoni mwa Ziwa Siljan lenye ufukwe mzuri wa kuogelea unaopakana na miamba pamoja na msitu mkongwe uliopangika na kukupa utulivu. Wakati mashamba mengi hapa Uswidi ni ya kisasa, leo hii Bockgården ni shamba dogo lililohifadhiwa vyema. Kuelekea magharibi na kusini mwa makaazi ya shamba, kwenye upinde hafifu kuelekea ziwani, kuna shamba la kilimo ambapo utajionea kondoo wa kigute (kondoo wenye asili ya Uswidi). Aidha, kuna msitu mdogo upande wa kaskazini. Mpakani mwa Rättvik na Orsa, kuna nyumba ndogo ya kiangazi na msitu ambao umekuwa ukimilikiwa na familiya yetu kwa vizazi na vizazi.

Haya ni baadhi ya mazingira tunayotamani kubadilishana nawe – Karibu Bockgården na ujisikie!

Kwa picha zaidi, tafadhali tizama "picha" za shamba la Bockgården!

 baringo

 Copyright 2010 Naturbruket Siljan