Je, unahudhuria kozi au programu ya uendeshaji wa maliasili na unatafuta mahali pa kufanya majaribio? Au je, unatamani kufanya kazi za mikono kwa bidii katika hali ya mazingira-rafiki na kuongozwa na maadili na misingi ya Permaculture? Kama ni hivyo basi, Naturbruket Siljan ni sehemu nzuri kwako!
Mbali na shughuli za kila siku za shambani, tungependa kuendeleza zaidi teknolojia mbadala za kiekolojia katika kaya. Hii ni namna moja ya kutafuta ufumbuzi mbadala shambani kama vile mfumo wa kuoka nyumba moto, umeme, maji, mfumo wa maji-taka na kutengeneza mboji.
Utakaribishwa kula chakula na kunywa chai nasi wakati wa mapumziko. Utapata chumba chako pekee na pia fursa nzuri ya kujifunza zaidi maisha ya kiekolojia.
Uwezekano mkubwa wa kufanya mazoezi kwetu ni kipindi cha kiangazi kwenye miezi ya Juni, Julai na Agosti.
Kwa picha zaidi, tafadhali tizama "picha" zinazohusu mazoezi!
Naturbruket Siljan ni chaguo lako – Wasiliana nasi!
Copyright 2010 Naturbruket Siljan |