tanzania_liten.gif spanien_liten.gifengland_liten.gifsverige_liten.gif
Tuelewe Utalii wa Mazingira Furushi la likizo Jinsi ya kufika Wasiliana nasi
logotyp.gif

Environment.jpg

Tunajali mazingira!

 

Ndiyo maana Naturbruket Siljan imefanikiwa na tunaendelea kujitahidi kutunza na kupiga vita uchafuzi wa mazingira. Jitihada hizi zinafanyika kwa njia mbalimbali kuanzia nyumbani, shambani hadi katika utoaji wa huduma kwa wateja wetu.

 

Je, ulikuwa unajua kuwa shughuli kuu ambazo zinawapa watu wengi furaha zaidi kwenye maisha yao pia hazina athari kubwa ya mazingira? Raha iliyoje hiyo! Ndiyo maana tunataka kuhamasisha mazingira yetu na sisi wenyewe kuwa na muda zaidi wa kuwa pamoja na uhusiano wa karibu zaidi na mazingira asilia katika njia muafaka na ya asili.

 

Kuna usemi usemao ”ukarimu huanzia nyumbani ila usiishie hapo”. Na hivi ndivyo tufanyavyo katika kuchangia kwenye mazingira yetu.

 

Nyumbani, kwanza kabisa tunajitahidi kupunguza matumizi yetu ya rasilimali hususan umeme. Hatupingi maendeleo ya teknolojia kiasi hicho ila hatuamini kama teknolojia pekee inatoa majibu katika changamoto za ulimwengu wetu. Wakati tunatumia umeme, tumeamua kuchagua umeme wa kijani, taa nyingi zao tutumiazo ni zinazotumia umeme mdogo, tunaanika nguo kambani badala ya kuzikausha kwenye mashine ya kukaushia nguo na tunaoka moto vyumba, kupasha moto maji na chakula kwa kutumia kuni zitokazo katika maeneo ya karibu.

 

Chakula, tunajitahidi kununua matunda na mboga kulingana na msimu, na tunatoa kipaumbele kwa vile vyakula vilivyothibitishwa kuwa na athari ndogo wakati wa kuzalishwa na vyakula vinavyozalishwa maeneo karibu. Tunakunywa maji safi ya mferejini (bombani) na tunaacha chakula kipoe kwanza kabla ya kukihifadhi kwenye jokofu au friza. Aidha kuhusu nyama, tunajitahidi kuepuka kula nyama zaidi ya inavyohitajika. Katika ardhi ya kilimo, ni vyema zaidi kuotesha mazao ya matumizi ya chakula cha binaadamu moja kwa moja kuliko kuotesha chakula cha wanyama tu. Tunaamini kwamba ni muhimu wanyama watunzwe kwa heshima, yaani waachiwe huru wafuate mwenendo wao wa asili bila ya kuwepo kwa shindikizo lolote linalochochewa na binaadamu. Kondoo wetu, mbali na kutupatia kitoweo, wanatusaidia kutunza mila, nyasi za asili katika hali nzuri.

 

Sisi tunashukuru kuwa na kipande cha ardhi, tunaamini kuwa kujitegemea kwa hali ya juu katika ngazi ya shambani kutafaidisha uhuru wetu, uchumi wetu binafsi na hususan mazingira yetu. Tumejiambia wenyewe kwamba tunaanza kidogo, tujitahidi kuthamini maendeleo yetu madogo wakati tukilenga malengo yaliyowazi na yenye kueleweka.

 

Jedwali lifuatalo linaonyesha baadhi ya maeneo tunayojitegemea kuhusiana na bidhaa ziingiazo na zitokazo shambani ambazo zimekisiwa kwa asilimia kwa mujibu wa mwaka zikionyesha wapi tulipofika na tunapolenga kufikia. Nambari katika mabano zinaonyesha kiwango cha kujitegemea kulingana na bidhaa zinazohitajika wakati wa uzalishaji.

 

Bidhaa/Mwaka

2008

2009

2010

2011

2012

2013

Mboga na bidhaa ziotazo ardhini kama vile viazi

20 (80)

25 (80)

30 (80)

35 (80)

40 (80)

45 (80)

Matunda mbalimbali

40 (60)

25 (60)

30 (60)

35 (65)

40 (70)

45 (75)

Viungo

5 (70)

10 (70)

15 (70)

20 (70)

25 (70)

30 (70)

Nafaka

0

0

0

0

0

0

Asali

0

0

0

80 (10)

90 (30)

100 (60)

Maziwa na bidhaa zake

0

0

0

0

0

0

Mayai

0

0

20 (10)

30 (30)

40 (60)

50 (60)

Kitoweo

50 (10)

100 (20)

100 (25)

100 (30)

100 (35)

100 (40)

Joto la nyumba*

60 (50)

30 (50)

60 (50)

30 (50)

70 (50)

70 (50)

 

*Umeme na kuoka moto vyumba, kupasha moto maji na chakula.

 

Usafiri unachangia sana kwenye uchafuzi wa hali ya hewa katika dunia yetu. Hata hivyo, tumefanikiwa kupunguza uchafuzi huo kwa njia tofauti. Baadhi ya njia hizo ni kama vile kuhakikisha tunatizama upepo kwenye maringi (matairi) ya gari unatosha, kuweka gia ya juu kidogo na kuepuka kupiga breki za ghafla au kuongeza spidi ghafla. Tunapendelea kuendesha gari kwa mwendo wa wastani. Aidha, tunapendelea zaidi kutumia usafiri wa jumla kama basi na treni, na tunajitahidi kutumia baiskeli na kutembea kadri inavyowezekana.

 

Tunajali mazingira na tunakuhamasisha uendelee kujali mazingira! Karibu uvumbue utalii wa mazingira na kujaribu Permaculture pamoja nasi!

 baringo

 Copyright 2010 Naturbruket Siljan