Tunafuraha kukujuulisha kuwa hivi sasa inawezekana kuja kuishi nasi katika shamba letu la kiikolojia la Bockgården baada ya ukarabati wa fleti na ngazi kwa ujumla!
Lengo letu mojawapo ni kukupa nafasi ya kujaribu kuishi katika shamba dogo hapa Uswidi (Sweden), kujaribu kuishi zaidi maisha ya kiikolojia na zaidi ya yote ufurahie maisha ya shamba! Shukurani zetu za dhati ziwafikie wale wote waliotusaidia, shukurani za pekee ziwaendee Naléns byggtjänst na mtandao wake, Bengt Larssons möbel och inredningssnickeri na zaidi ya wote mjomba wetu, Roine.
Tunazishukuru pia familia zetu husika, marafiki na wageni wetu kwa kuwepo kwenu kutupa moyo na uvumilivu wao katika kipindi hiki!
Januari 2010.
Copyright 2010 Naturbruket Siljan |