tanzania_liten.gif spanien_liten.gifengland_liten.gifsverige_liten.gif
Tuelewe Utalii wa Mazingira Furushi la likizo Jinsi ya kufika Wasiliana nasi
logotyp.gif

Ethics1.jpg

Maadili

Tunachukua kozi ya miaka miwili ya ubunifu wa kilimo cha kudumu ”Permaculture” kupitia Permaculture Association Britain. Permaculture inatuongoza katika maadili na ubunifu wa misingi ambayo tunajitahidi kuifuata kadri ya uwezo wetu.

’Maadili na Misingi

”Tukitaka kuendelea zaidi, kuunda mbinu endelevu na kuinua kiwango cha maisha ni muhimu kufahamu asili za ulimwenguni na kuishi nazo kwa utulivu na ubunifu – kufahamu kuwa sisi ni sehemu ya utando wa dunia, sio kujitenganisha nayo”. Permaculture inajumuisha utaratibu wa maadili na misingi ambayo tunalenga kutekeleza kwa vitendo. Hii inalenga kwenye uendelevu na usawa, na kwa ujumla imegawanyika katika mafungu matatu:

Kuujali ulimwengu

Permaculture ikiwa ni muundo wa utaratibu unategemea mbinu asilia. Ni kuhusu kufanya kazi na mazingira asilia sio kinyume chake – sio kutumia maliasili kiholela au kwa kiwango kisichoweza kujifidia. Inamaana pia kutumia bidhaa zitokanazo kwenye mfumo mmoja kama ni malighafi kwa mfumo mwengine (kwa mfano, mabaki ya mbogamboga kuwa mbolea) hivyo kupunguza takataka.

Kuwajali watu

Kujali watu na kutuangalia sisi kama watu, sio tu dunia tunayoishi. Inahusika kwa ngazi zote, kuanzia ya watu binafsi hadi jamii. Kujitegemea, ushirikiano na kusaidiana inastahili kusisitizwa. Hata hivyo, ni muhimu zaidi tujitizame katika ngazi ya watu binafsi pia. Ujuzi wetu hauwezi kumsaidia mtu yeyote ikiwa sisi wenyewe tumechoka kufanya kitu chenye faida! Kujali watu pia ni kuhusu urithi wetu kwa vizazi vijavyo.

Mgawanyo sawa

Sehemu ya mgawanyo sawa kwenye maadili ya Permaculture ni kukumbanisha kuujali ulimwengu na watu pamoja. Tuna ulimwengu mmoja tu, na inabidi tugawane miongoni mwetu, viumbe hai vyengine na vizazi vijavyo. Hii inamaana kuwa na kikomo cha matumizi hususan ya maliasili na kuwezesha kila mtu kupata mahitaji muhimu ya maisha – maji safi, hewa safi, chakula, makaazi, kazi yenye maana na maingiliano ya kijamii na watu wengine.

Permaculture haitupi suluhu maalumu ya kutatua matatizo yanayoikabili dunia – hamna mtu yeyote atakaekuomba uoteshe mitishamba katika sehemu ya chini kabisa ya pembe ya bustani yako au uvae nguo zilizofumwa kwa mikono kutokana na malighafi zilizotumika, zisizochobuliwa, zilizomahuluku wala kuuzwa kwa kupitia mfumo wa biashara-sawia. Permaculture inahusu zaidi kukupa uhuru wa kuzingatia mazingira yako na kufanya maamuzi sahihi yanayokuhusu kwa mujibu wa hali yako kwa kutumia malighafi ulizonazo.”

Maelezo zaidi kuhusu Permaculture yanapatikana kwenye tovuti ya Permaculture Association Britain ambapo pia tumenukuu maelezo ya hapo juu.

 baringo

 Copyright 2010 Naturbruket Siljan