Karibu ukae nasi kwenye shamba letu la kizamani lakini maalumu, Bockgården – sehemu ambayo utapata huduma za kinyumbani na za kibinafsi. Amani na utulivu wa Bockgården, na upepo mwanana kutoka Ziwa Siljan vitakufanya ujihisi kupumzika na kuthamini mazingira ya asili! Tuna fleti, vyumba vya kiangazi na nafasi za mahema.
Fleti ina mandhari mazuri ya Ziwa Siljan na kuna jiko, jiko maalum litumialo kuni na jokofu, maji ya moto na bafu.
Pia tuna vyumba kadhaa vya msimu wa kiangazi vyenye samani zikijumuisha vitanda.
Hema lako litapata mandhari mazuri kabisa ya msitu, machunga, shamba na maji. Kwa hapa Bockgården utaweza kutumia choo cha nje, kupata maji safi ya kunywa, umeme na kukoga kwa burudani kwenye majabali ya Siljan.
Tafadhali tunaomba usivute sigara au kuingiza wanyama wa nyumbani ndani ya nyumba.
Mwaka mzima
Muda wa kujiandikisha ni kuanzia saa 9 mchana na muda wa kutoka sio zaidi ya saa 4 asubuhi ya siku ya kuondoka.
Kiswahili, Kiingereza, Kihispania na Kiswidi
Chakula safi, cha kiekolojia kinapatikana kama ukihitaji.
Kifungua kinywa; Krona 65/mtu
Furushi la chakula cha mchana; Krona 65/mtu
Chakula cha jioni; Krona 80/mtu.
Idadi ya watu/ Kipindi |
1 Jan. - 11 Feb. 6 Machi - 10 Juni 21 Agosti - 31 Dis. |
12 Feb. - 5 Machi 11 Juni - 20 Agost |
Mtu 1 |
Krona 450/siku |
Krona 840/siku |
Watu 2 |
Krona 600/siku |
Krona 840/siku |
Watu 3 |
Krona 750/siku |
Krona 1050/siku |
Watu 4 |
Krona 900/siku |
Krona 1260/siku |
Watu 5 |
Krona 1050/siku |
Krona 1470/siku |
Vyumba vya kiangazi: Krona 150/kitanda
Mashuka na taula: Krona 120/kitanda
Hema: Krona 100/siku
Umeme: Krona 50/siku/muungo.
Watoto chini ya miaka mitatu, bure!
Long-distance skates; Krona 150/siku
Snow-shoes: Krona 150/siku
Boti; Krona 200/siku
Baiskeli; Krona 100/siku
Licha ya shughuli mbalimbali ambazo Naturbruket Siljan zinazokuandalia, kuna shughuli nyingi za kiutamaduni zinazoendelea karibu na shamba. Soma taarifa zaidi ya shughuli hizi kupitia http://www.siljan.se/en/.
|
Copyright 2012 Naturbruket Siljan |