Kama unakuja kwa gari, baiskeli au mguu, kaskazini tu mwa Rättvik, pinda kushoto kuelekea Sjurberg na fuata hiyo barabara ya zamani kwa takribani kilomita 2. Mwishoni mwa kijiji cha Sjurberg, ambapo kuna mkunjo mkali, utaona kushoto kwako njia isiyo na lami na kibao kimeandikwa ’Bockgatan’. Tupo mwishoni mwa hiyo njia. Ukitaka kujua kama umefika mahala sahihi utaona uzio wa kondoo, uzio wa kiutamaduni wa boriti uliozunguka nyumba na Ziwa Siljan.
Unaweza pia kuja kwa basi mpaka Bockgården! Kutoka Rättvik, panda basi nambari 70 au 72 mpaka kituo cha ’Mårsgården’ (Moshgoden). Rudi nyuma kidogo kwenye mkunjo mkali, kulia kwako utaona kibao kimeandikwa ’Bockgatan’. Fuata huo ujia. Inachukua si zaidi ya dakika 5 kutoka kituoni mpaka shambani, Bockgården.
Tunategemea tutaonana Bockgården!
Copyright 2010 Naturbruket Siljan |