Naturbuket Siljan na mazingira yake yatakusaidia kuja karibu na asili. Hapa kuna uwezekano wa kukodi baiskeli, mtumbwi (kipera) au malazi mazuri ya farasi wako. Wakati wa msimu wa kipupwe kunapatikana vyombo vya kuendesha kwenye barafu (kama vile kick-sledge, skiis na ice-skates) ikiwa ni sehemu ya starehe kwa ajili yako ili uvumbue maumbile asili juu na kuzunguka Ziwa Siljan.
Kuna njia nzuri za matembezi, kuendesha farasi na baiskeli. Njia ya matembezi ya Siljan inapita upande wa magharibi tu wa shamba katikati ya msitu tulivu wakati njia za farasi na baiskeli zinapita mashariki tu mwa shamba.
Ukija na farasi, tutakuandalia kiasi cha kuhakikisha kuwa hata farasi wako atajihisi amekaribishwa! Usijali kuhusu mbwa mwitu, dubu na paka pori kwani tuna uzio maalum unaokinga wanyama walao nyama.
Kitabu ‘Sjurberg – en Rättviksby förr och nu’ (Sjurberg – Kijiji hapo awali na sasa) kinapatikana kwa ajili ya kukusaidia katika mizunguko yako kipindi utakachokaa nasi. Unaweza kuvumbua kijiji wewe pekee! Kitabu kikiwa na ramani ya kijiji kinapatikana kwa kiswidi tu ila tunaweza kukupasha yaliyomo kabla hujafuata asili.
Kwa picha zaidi, tafadhali tizama "picha" za Fuata Asili!
Ukitaka kukaa nasi, utapata maelezo zaidi kwenye ‘Malazi’
Copyright 2010 Naturbruket Siljan |