tanzania_liten.gif spanien_liten.gifengland_liten.gifsverige_liten.gif
Nyumbani Malazi Shughuli Chakula Permaculture Zanzibar Kuhusu sisi Wasiliana nasi
logotyp.gif

Speciella hembakade bröd

Chakula

 

Furahia ladha nzuri ya chakula chako!

Tunapanua ukarimu wetu pia kwako wewe unayependa chakula kizuri. Sote tunafahamu kama chakula ni muhimu kwenye maisha yetu. Labda ndiyo sababu tunafurahia kuwa na chakula kizuri. Chakula kizuri tunachojua wapi kinapozalishwa, chakula ambacho ni sehemu ya mzunguko asilia bila ya kemikali zisizo na msingi. Chakula hicho, kwa bahati mbaya kimekua adimu. Tunazalisha chakula ambacho sisi wenyewe tunakula. Kwa ajili ya kuwapatia watu wengi zaidi chakula hicho adimu, tunajaribu kadri ya uwezo wetu kuzalisha shambani kwetu ili nawe upate sehemu yako ya chakula kizuri.

 

Tunakupatia chakula cha mbogamboga. Msemo wetu ni taratibu ndio mwendo. Umeshawahi kuujaribu mkate wetu wa ‘rye’ ambao umepikwa masaa nne kwa mvuke? Vyakula tunavyokukaribisha mara nyingi vimetoka kwenye bustani yetu ya mbogamboga, bustani yetu ya viungo au kutoka kwenye bustani ya jirani yetu ya matunda. Chakula tunavyokitayarisha mara nyingi hutokana na utamaduni wa familiya zetu. Tunakuahidi kuwa mikate yote tunaioka/ kuipika kwa jiko la kuni tunaitayarisha kwa uangalifu mkubwa na kwa mapenzi kiasi cha kwamba hata wewe, kama ni mgeni wetu, una uwezo wa kufaidi mkate halisi na mtamu.

 

Unaweza kufaidi chakula chetu zaidi hapa Bockgården kwa kipindi utakachokaa nasi, kushiriki kwenye kozi zetu au kuja kwenye duka letu la shambani. Chakula kinakuwa kitamu zaidi pale mzalishaji na mnunuzi wanapokutana macho kwa macho.

 

Ukitaka kujua zaidi, usisite kuwasiliana nasi!

 

 Copyright 2012 Naturbruket Siljan